Kilio cha muda mrefu cha wasanii wa Tanzania sasa kimefika kikomo baada ya wadau kujitokeza na kuanzisha tuzo ambazo zinaitwa Bantu Film Awards zinategemewa kufanyika mwezi ujao katikati tarehe na siku tutawajuliisha kupitia blog yako ya The Greatest, leo kulifanyika mkutano na waandishi wa habari katika hotel ya Serena kuzungumzia tuzo hizo, embu twende tuone mambo yalivyokuwa.....
Ulifika muda wa Jb kuongea yake machache kuhusu tuzo za Bantu, Kubwa alisisitiza kuwa umefika muda sasa ya wasanii kufanya kazi zenye ubora wa Kimataifa maana hiki ndicho kilkuwa kilio chetu cha muda mrefu sana maana hata wanafunzi wanapokuwa wanasoma lazima mwisho wa mwaka ukifika wanafanya mitihani kama kipimo cha mwaka mzima alichosoma na ndio maana leo nasi tumekuwa na kitu kama hiki cha kujipima kuwa ndani ya mwaka mzima umefanya kitu gani.
Hayo yalikuwa ni maneno ya Jb akiwawakilisha wasanii wa Tanzania nzima..
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa tayari kuanza mkutano na waandishi wa habari.
The Greatest, Richie na Jb wakimfuatilia mratibu wa tuzo za Bantu Film awards bwana Stewart akifafanua jinsi tuzo zitakavyokuwa
Irene Uwoya naye alikuwepo amesema kuwa amepania kuzoa tuzo za mwaka huu..
Tukiwa makini kufatilia kikao na mambo yatakavyokuwa.
Stewart ndiye Mratibu wa Bantu Film Awards
Stewart akiendelea kutoa ufafanuzi jinsi tuzo za Bantu zitakavyokuwa kwa waandishi wa habari
Safi sana kwa kweli wasanii wa Tanzania tumekuwa na faraja kubwa juu ya tuzo hizi za Bantu
Mambo yakiendelea........
Jb mwenyekiti wa Bongo Movie
The Greatest
Irene Uwoya
Single Mtambalike
CLIC HERE TO READD MORE
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
MWIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA, WEMA SEPETU AONYESHA JUMBA LAKE
UNAJIFUNZA NINI KAMA MDAU WANGU WA BLOGU HII?
CHALLENGE KWA WATU WANGU WA UPANDE WA KRISTO, NA SISI TUCHEZE FILAMU NINI ILI TUTOKELEZEE NA MIJENGO...HAHAHAHA!!!
Wema Sepetu, mwigizaji wa filamu Tanzania
ANGALIA PICHA ZINGINE BOFYA HAPA
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
11 June 2012
ODAMA NDANI YA HOT MIX-EAST AFRICA
Msanii wa filamu Tanzania Jeniffer Kyaka a.k.a ODAMA wiki
iliyopita alifanyiwa mahojiano na EATV kuhusiana na filamu yake mpya
ya RUDE inayofanya vizuri sokoni kwa sasa. Mbali na hivyo alielezea
maisha yake kwa ujumla na jinsi alivyofaidika na kazi ya filamu.
Kutoka kushoto ni mtangazaji wa Hot Mix, Anna Mbanjo,
akifuatiwa na msanii wa filamu, Jeniffer Kyaka (Odama) na Fatna Ramole
wa Hot Mix wakiwa katika studio za EATV
Jennifer Kyaka mbali na uingizaji pia ni Mkurugenzi wa
kampuni yake ya J-FILM 4 LIFE iliyoko Biafra Kinondoni Dar es Salaam.
Aliongeza kwa kusema mbali na kucheza filamu za watu wengine na pia
ametengeneza filamu katika kampuni yake ya J-FILM 4 LIFE kama The
Avenger, Life 2 Life, All About Love, Loreen, RUDE na filamu mpya
nyingine ambayo inakuja karibuni inayoenda kwa jina la HOUSE MAID .
Odama akiwa katika pozi baada ya kufanya interview
Odama alimaliza kwa kuwashukuru wapenzi wake wanaom-support kwa kununua filamu zake, na hasa wanaotembelea blogu yake ( www.odama1.blogspot.com) ambayo imekuwa gumzo kubwa kwa kukusanya matukio ya wasanii wa filamu Tanzania na nje ya nchi.
Wakitokelezea ndani ya EATV
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
6 May 2012
BREAKING NEWS6 May 2012
FILAMU KWAAJILI YA KUMCHANGIA MWIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA SAJUKI ANAYETIBIWA NCHINI INDIA KUANZA LEO JUMATANO .
Zamaradi wa akiongea mjengoni Clouds FM katika kipindi cha Leo Tena, amesema filamu hiyo itawahusisha mastaa wa Tanzania kama wachezaji filamu, watangazaji, waimbaji , viongozi wa serikali kama mbungu Mdee, wachezaji wa mpira, undergrounds, maproducer na wengine wote, kwa ujumla ni ma-celebrity wote wa Tanzania. Zoezi hili linaanza leo. Kama ungependa kuwa mojawapo wasiliana na Clouds FM au kutana na Zamaradi Mtetemo Clouds FM
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire